BENCHI la ufundi la Azam FC lililo chini ya Kocha Mkuu Aristica Cioaba limepandisha majembe sita ya kazi kutoka timu ya vijana ya umri wa miaka 20 (Azam U 20) na kufanya mazoezi kwenye kikosi cha wakubwa leo. Azam FC inafanya mazoezi yake kwenye uwanja wao wa Azam Complex ambao nyasi zake zimefanyiwa maboresho hivi karibuni na kuingia kwenye anga za kimataifa zaidi. Wachezaji hao sita ambao wamepandishwa leo na kufanya mazoezi na wakubwa ni pamoja na Emmanuel Kabelege, Shaban Kingazi, Omary Banda, Pascal Msindo, Samwel Onditi, Abdallah Madirisha.