Hitmaker wangu ngoma ya #DODO#SO HOT na nyinginezo @officialalikiba ameonyesha kufurahishwa na kitendo cha @rayvanny Kuimba wimbo wake wa Dodo na kusema kuwa Dodo ni ngoma anayeikubali sana kutoka kwa Alikiba.

Akiongea na Bongo5 Alikiba ameonyesha kufurahishwa na Rayvanny na kusema kuwa anamshukuru sana kwa kuonyesha kuwa yeye ni mdau wa muziki wa Bongo Fleva.

Alikiba aliongeza kuwa “Hata mimi nafatilia sana muziki wa Rayvanny kwa sababu ni mbunifu, Napenda baadhi ya nyimbo zake ikiwemo ‘Kwetu’ na ‘Nitokeje’ mfano kwetu nishawahi kuimbaga kipindi cha nyuma, Muziki mzuri una siri kubwa sana utaimba hata ukiwa chooni”

The post Alikiba – “Nasikiliza na kufuatilia muziki wa Rayvanny kwa sababu ni mbunifu” (+Video) appeared first on Bongo5.com.