ADO Shaibu Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo amesema Serikali ilimtaka alipe Shilingi 123 Milioni kama faini ya kushindwa kesi aliyomshtaki Rais John Magufuli.

Katibu Mkuu huyo alimshtaki Rais Magufuli kwa kumteua Dk. Adelardus Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kudai kuwa kitendo hicho ni kinyume na katiba ya nchi kwakuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali anatakiwa kuwa amehudumu katika nafasi uwakili kwa muda wa miaka 10 hivyo Kilangi hakufikia hatua hiyo.

Mahakama ilitupilia Mbali shauri hilo tarehe 20 Septemba mwaka 2019 ambapo Serikali iliiomba mahakama imuamuru alipe faini .

Leo tarehe 7 Juni 2020, Ado Shaibu amewaambia waandishi wa Habari kuwa Serikali iliiomba mahakama iamuru alipe kiasi cha shilingi 123 Milioni kama fidia kwa kushindwa kesi.

Ado ametanabaisha kuwa hatua hiyo ya serikali ilikuwa ikilenga kumkatisha tamaa yeye na wanaharakati wengine wenye kutaka kuiwajibisha serikali mahakamai kwa kutaka alipe kiasi kikubwa cha fedha kama fidia