CHAMA cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania kimesema, kimeupokea kwa mikono miwili mwaliko uliitolewa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). 

Kauli hiyo ya ACT-Wazalendo wameitoa leo Alhamisi tarehe 4 Juni 2020 ikiwa ni siku moja imepita tangu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika atangaze kufungua milango ya ushirikiano kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020. 

Jana Jumatano, Mnyika akizungumza na wanadishi wa habari makao makuu ya Chadema Kinondoni jijini Dar es Salaama alisema, wamefungua milango ya majadiliano na vyama vingine vya siasa ambavyo vinadhamira ya kweli ya kushirikiana kuiondoa CCM madarakani. 

Leo Alhamisi tarehe 4 Juni 2020, MwanaHALISI ONLINE limezungumza na Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu juu ya kauli hiyo ya Chadema ambapo amesema, “ACT- Wazalendo tupo tayari kushirikiana na vyama makini vya upinzani.”