Msanii wa BongoFleva Alikiba, amefunguka kusema wimbo wake bora kabisa anaoupenda ni "My Everything" iliyotoka miaka 8 iliyopita, pia amesema mwaka 2020 amebadilisha upepo wa muziki kwani anataka kwenda sawa na mashabiki zake.


Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio, wakati anatambulisha kazi yake mpya ya "So Hot" Alikiba amesema.

"Wimbo wa My everything naupenda, una spirit ya kipekee ukiuliza kuhusu mapenzi unaweza usiwe na majibu, ndiyo maana wanasema mapenzi majani huota popote, labda nitapenda mwingine zaidi ya huo, nina mpango wa kuifanyia video na kuifanya upya iwe ya kisasa" amesema Alikiba.

"Hata ukiicheza mara Laki 1 nitaicheza na nitaifurahia, wakati mwaka 2020 unaanza nimebadilisha upepo wa muziki wangu, huu ni mwaka wa kipekee na kila mtu alikuwa na target zake mi nilikuwa nataka niende sawa na mashabiki zangu" ameongeza.