Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein amesema serikali inakusudia kulegeza masharti  yaliyowekwa Zanzibar ya kupambana na maradhi ya virusi vya Corona wakati wowote kuanzia sasa.

Rais Shein ametoa kauli hiyo katika salamu zake za Eid kwa wananchi wa Zanzibar baada ya kumalizika kwa mwezi Mtukufu wa Ramadhan ambapo amesema hali ya sasa ni nzuri ambapo Zanzibar ina wagonjwa 34 tu.