Zambia imechukua hatua za kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona kwa kufunga mpaka wake na nchi jirani ya Tanzania kuanzia Leo Jumatatu. Hii ni baada ya kuwa na maambukizi mengi, hususan miongoni mwa wafanyabiashara wa ngono na madereva wa Malori kwemnye miji ya mipaka nchini humo.

Hatua hiyo inajiri baada ya taifa hilo kuripoti wagonjwa 76 wa virusi vya corona katika mji uliopo katika mpake wake na Tanzania

Kufikia sasa taifa hilo limethibitisha wagonjwa 367 wa virusi vya corona nchini humo.

Akizungumza kwa niaba ya rais wa taifa hilo, Edgar Lungu Waziri wa afya nchini humo Chitalu Chilufya alitangaza kwamba mpaka huo utafungwa kwa muda .

Alisema kwamba hatua hiyo itatoa fursa kwa mikakati mipya ya kukabiliana na virusi hivyo kuwekwa.

Katika muda huo, amesema wafanyakazi wa uhamiaji katika mpaka huo watapatiwa mafunzo mapya ya jinsi ya kuhudumia mizigo na raia wanaoingia.

”Hali kule Nakonde ni mbaya na hii leo rais Edgar Lungu ana wasiwasi , Hivyobasi ameagiza kuanzia Jumatatu tarehe 11 mwezi Mei 2020, mpaka wa Nakonde utafungwa kwa muda , hakutakuwa na usafiri ndani na nje ya mpaka huo na vilevile hakutakuwa na usafiri viungani mwa eneo hilo ili kuwezesha utekelezwaji wa mikakati inayolengwa ikiwemo kuwapa mafunzo mafisa wetu mpakani”, alisema waziri huyo wa Afya.

Amesema kwamba maafisa hao vilevile watapatiwa vifaa vya kujilinda dhidi ya ugonjwa huo huku vifaa vya karantini vikiwekwa kwa lengo la kuwalinda maafisa na wakaazi wa Nakonde

Tanzania yalaumiwa kuhusu jinsi inavyokabiliana na corona

Taifa la Tanzania limethibitisha wagonjwa 509 wa virusi vya corona huku wagonjwa 183 wakipona na 21 wakiripotiwa kufariki kutokana na virusi hivyo.

Serikali ya Tanzania imelaumiwa katika mikakati yake ya kukabiliana na virusi hivyo huku rais John Pombe Magufuli akitilia shaka vifaa vya kuwapima wagonjwa.

baadhi ya viongoxi wa kidini wamesitisha ibada, lakini wengine wengi bado wanajumuika pamoja kila Jumapilibaadhi ya viongoxi wa kidini wamesitisha ibada, lakini wengine wengi bado wanajumuika pamoja kila Jumapili

Tofauti na nchi nyingi, Tanzania haijachukua hatua kali za kupiga marufuku watu kutoka nje ijapokuwa mikusanyiko mikubwa ya watu kama misiba na harusi imepigwa marufuku.

Lakini usiri wa mazishi yaliyopigwa picha unachochea hisia kuwa ukubwa haswa wa maambukizo nchini humo unafichwa.

Kipaumbele kikuu cha serikali ya Tanzania ni kutoumiza uchumi wa nchi huku rais Magufuli akipinga kulifunga jiji la kibiashara la Dar es Salaam.

Katika hotuba yake kwa taifa rais wa Zambia Edgar Lungu siku ya Ijumaa alitangaza kufunguliwa kwa maeneo ya kufanyia mazoezi na casino huku akitoa wito kwa wanasayansi nchini humo kutafuta suluhu ya kinyumbani katika vita dhidi ya ugonjwa huo.

Hatahivyo aliamrisha kwamba klabu za burudani zitaendelea kufungwa hadi atakapotangaza tena.

 

https://bit.ly/2SS74kH

The post Zambia yatangaza kufunga mpaka wake na Tanzania kisa Corona, Fahamu zaidi appeared first on Bongo5.com.