Zoezi la kupima watu ni jukumu kubwa katika kukabiliana na virusi vya corona kwasababu kunasaidia kujua ugonjwa huo umesambaa kwa kiasi gani.

Kituo cha Kudhibti Magonjwa Afrika ambacho kinaratibu mutukio ya kupambana na janga la corona kote barani, kinasema kuna pengo kubwa kwenye kasi ya upimaji kati ya mataifa.

Kwahiyo ni nchi gani zinazofanikiwa katika upimaji na zipi bado zimeachwa nyuma?

Nchi gani zimefanikiwa kupima watu wengi au vyenginevyo?

Baadhi ya Mataifa madogo ya Afrika yamepiga hatua kubwa katika kupima kuthibitisha walioambukizwa ikilinganishwa na mataifa jirani makubwa.

Mauritius na Djibouti, kwa mfano, yote yamefanikiwa kupima kiasi mkubwa cha watu ikilinganisha na idadi ya watu.

Ghana pia imesifiwa kwa kiwango chake cha upimaji, ambacho serikali yake inasema kutasaidia kudhibiti maambukizi ya virusi punde tu baada ya kulegezwa kwa masharti ya kusalia ndani.

Afrika Kusini pia nayo imekuwa na mkakati imara unao hakikisha raia wanapimwa na hadi kufikia sasa watu 200,000 wamefanikiwa kupimwa.

Lakini idadi hiyo ni ya chini mno ikilinganishwa na nchi kama vile Korea Kusini, Italia na Ujerumani.

Kuna wasiwasi kwamba nchi ya Nigeria yenye idadi kubwa ya watu Afrika, haipimi kiasi ya watu kinachohitajika ingawa serikali inasisitiza kwamba inafuatilia walioathirika kwa misingi ya vile mgonjwa anavyoumwa.

Social distancing in Uganda

Mwandishi wa BBC Nigeria Chi Chi Izundu anasema, mamlaka inaongeza kiwango cha upimaji.

“Lengo ni kupima watu 5,000 kwa siku – lakini hawajafikia hata watu 1,000.”

Pia ni sawa kuongeza kwamba baadhi ya nchi katika bara hili hazina takwimu za wanaopimwa kama vile Eritrea na Algeria.

Mataifa mengine hayana uwezo wa kupima huku mengine kwasababu mbalimbali zimekataa kutoka takwimu zao.

Kwa mfano, Tanzania Rais Magufuli amesema kutoa taarifa kama hizo kuna kunatia wananchi hofu.

Nchi yake imekuwa ikitoa taarifa baada ya muda kiasi na wakati mwengine inatoa tu idadi ya watu waliopona kutokana na virusi pekee.

Changamoto katika upimaji ni zipi?

Kupata kemikali zinazotumika kwenye mchakato wa kupima ni changamoto kwasababu nchi za Afrika hazitengenezi kemikali hizo hivyobasi zikishindania kusambaziwa sawa na nchi zingine kote duniani.

John Nkengasong kutoka Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika anasema, ukosefu wa ushirikiano ulimwenguni na umoja umetikisa Afrika katika suala zina la kubaini ikiwa mtu ameambukizwa virusi vya corona.

Anasema nchi za Afrika huenda zikawa na pesa lakini nchi 70 zimeweka masharti ya uuzaji wa dawa nje na kufaanya iwe vigumu kununua bidhaa za msingi.

Nigeria coronavirus outbreakMtu akiwa amebeba kipeperushi cha Nigeria, kinachoelezea watu namna ya kusitisha maambukizi ya virusi vya corona

Pia kuna vikwazo vyengine katika kuongeza idadi ya wanaopimwa, ikiwemo hatua ya kusalia ndani kupunguza usafiri, ambako kunafanya iwe vigumu kwa watu kufika kwenye maeneo ya kupimwa.

Hata hivyo, Ngozi Erondu, mshiriki wa kituo cha Afya cha Chatham House, anasema tatizo kubwa ni vifaa.

“Wala sio kuwa na kemikali nyingi,” anasema Dkt. Erondu.

Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia magonjwa Nigeria, kwasasa kina maabara 18 ambazo zinaweza kupima na kubaini ikiwa mtu amemabukizwa vuris vya corona au la.

Lakini kwasasa maabara hizo zimetoa maombi ya haraka ya kupata vifaa muhimu vya upimaji.

Kenya pia imekubali kuwa na changamoto ya kupata vifaa vya kupima kwa ujumla na matokeo yake, idadi ya wanaopimwa imepungua kwa kiasi kikubwa.

Afisa mmoja alisema katika siku za hivi karibuni imekuwa na vifaa 5,000 pekee vya kupima watu kote nchini humo na kwamba wanatarajia vifaa vyengine 24,000.

A meeting in Lagos State to plan for tackling coronavirusMkutano katika mji wa Lagos nchini Nigeria wa kupanga namna ya kukabiliana na virusi vya corona

Pia kuna sababu zengine za kijamii na kisiasa ambazo huenda zikawa kizuizi cha watu wengi kupimwa kwa siku.

“Katika baadhi ya jamii huenda watu walioathirika na virusi vya corona wakanyanyapaliwa,” amesema Ngozi Erondu. “Hiyo pia huenda ikawa sababu viongozi katika jamii huenda wasililitilie mkazo suala zima la upimaji hasa kwa wale ambao huenda wakataka kuchagukuliwa tena.”

Umoja wa Afrika na Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika wameanzisha mradi unaofahamika kama Ushirikiano wa Kuharakisha Upimaji wa Covid-19, ambako kunaangazia kufuatilia, kupima na kutambua walioambukizwa.

Mradi huo unalenga kuanzisha karibia kupima watu milioni moja kwa wiki nne kote barani.

Mlipuko ya kwanza ya virusi vya corona barani Asia na Ulaya kuliwapa mataifa ya Afrika muda wa kufikiria hatua watakazochukua na tajriba ya kukabiliana na janga kama vile Ebola pia imesaidia.

Lakini kupata vifaa vya kupima katika dunia yenye ushindani mkubwa kupima kwa wakati stahiki na kuwa na maabara za kubaini waliopata maambukizi sio zoezi rahisi kwa nchi ambazo uchumi wao ni wa chini na mfumo dhaifu wa afya.

The post Yafahamu mataifa ya Afrika, Yaliyotajwa kufanya vizuri katika upimaji wa virusi vya Corona appeared first on Bongo5.com.