Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema mlipuko wa #CoronaVirus unaweza kusababisha vifo kwa Waafrika wapatao 190,000 ndani ya mwaka mmoja tangu uanze, kama ukishindwa kudhibitiwa.
Mkurugenzi wa WHO-Afrika, Dkt. Matshidiso Moeti amesema kuna uwezekano kuwa #COVID19 haitosambaa kwa kasi barani humo kama ilivyokuwa kwa mataifa mengine duniani.
Hata hivyo, amezitaka Serikali kuweka mikakati ya kupima #Corona, kuwatibia wagonjwa, kuweka wenye maambukizi karantini na vilevile kutafuta wale waliokuwa karibu na wagonjwa wa Virusi hivyo.
Awali, WHO ilitabiri Waafrika Milioni 29 hadi 44 wanaweza kupata #COVID19 kwa mwaka mmoja na Milioni 5.5 wanaweza kuhitaji tiba Hospitali, idadi ambayo ni kubwa kuliko uwezo wa sekta za afya katika nchi nyingi.
The post WHO: Waafrika 190,000 wanaweza kufa kwa mwaka kutokana na Corona appeared first on Bongo5.com.