Msemaji wa Shirika la afya duniani (WHO) Bibi Fadela Chaib jana kwenye mkutano na waandishi wa habari amesema, kwa mujibu wa ushahidi uliopo sasa, WHO inaamini kuwa virusi vya Corona vinatoka kwa wanyama.

“Ushahidi wote tulionao unaonesha kuwa virusi vya Corona vinatoka kwa wanyama, na havitokani na uingiliaji wa binadamu au kutengenezwa kwenye maabara.”

Vilevile amesema WHO inapambana na maambikizi ya virusi pamoja na uvumi. 
 
“WHO inapambana na kuenea kwa virusi vya Corona duniani, wakati huo huo inapambana na kuenea kwa habari feki duniani. Wakati virusi vipya kama virusi vya Corona vinapotokea, habari nyingine feki huenea kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.”- Alisema