Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Innocent Bashungwa Pamoja na Waziri wa Afya  Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu wameendesha Kikao cha Wadau kujadili upatikanaji na uzalishaji wa vifaa kinga kwa ajili ya kujikinga na COVID – 19 jana  tarehe 13.05.2020 jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa amewapongeza wamiliki wa viwanda hivyo kwa kubuni na kugundua teknolojia na uzalishaji wa  vifaa kinga kwa ajili ya kupambana na ugonjwa huo.

“Kuanzisha viwanda ni sehemu ya ulinzi wa nchi,hivyo kuwa na viwanda vyetu nchini hususani wakati wa shida imesaidia upatikanaji wa baadhi za vifaa kinga kwa bei nafuu”.Alisema Waziri Bashungwa

Waziri Bashungwa ameitaka  MSD kununua vifaa kinga vinavyozalishwa na viwanda vya ndani ambavyo vimekidhi viwango na vimesajiliwa na TMDA badala ya kutumia fedha iliyotengwa na Serikali kununua vifaa hivyo nje ya nchi.

Waziri Bashungwa ameahidi kukitembelea kiwanda cha Msagala Investment kilichopo Bagamoyo ambacho kinatarajia kuanza kuzalisha malighafi za utengenezaji wa barakoa kutokana na pamba zinazolimwa nchini.

Amesema katika kikao hicho wamekubalia kujipanga vizuri katika uzalishaji wa vifaa kinga na hivyo wamewataka Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kujikita katika kuzalisha barakoa aina ya N95 na glove kutokana na kwamba viwanda vya namna hii havipo nchini.

Pia Waziri Bashungwa ameitaka TMDA kushirikia na wizara ya viwanda kuisaidia NDC kuweza  kufanya kiwanda hicho kuanza kuzalisha kwa wakati na hivyo kusaidia watumishi wa afya walio mstari wa mbele kutoa huduma bila hofu.

Kwa upande wa MSD, Waziri Bashungwa ameitaka  kununua vifaa kinga vinavyozalishwa na viwanda vya ndani ambavyo vimekidhi viwango na vimesajiliwa na TMDA badala ya kutumia fedha iliyotengwa na Serikali kununua vifaa hivyo nje ya nchi.

Waziri Bashungwa ameahidi kukitembelea kiwanda cha Msagala Investment kilichopo Bagamoyo ambacho kinatarajia kuanza kuzalisha malighafi za utengenezaji wa barakoa kutokana na pamba zinazolimwa nchini.

Katika kuchukua hatua zaidi, Waziri Bashungwa amewasihi wazalishaji wa vifaa tiba kuongeza jitihada za kuzalisha ili kuendana na kasi ya soko Pamoja na kuhakikisha Watanzania wanakuwa salama kipindi hiki cha COVID-19

Pia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. John Pombe Magufuli kwa kuhimiza sera ya Tanzania ya Viwanda kwani sera hiyo imekuwa ya manufaa sana hasa kipindi hiki cha COVID-19 kwani vifaa vingi vinazalishwa hapa ndani bila kutegemea kuagiza kutoka nje ya nchi.

 “Rais aliona mbali, kuwa na viwanda vyetu hapa nchini hata wakati wa shida, viwanda hivi vingekuwa havipo tungepata shida sana,”Amesema Bashungwa.

Katika hatua nyingine, Waziri Bashungwa amempongeza Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kwa hatua Madhubuti anazozifanya katika kukabiliana na COVID-19

“Nakupongeza sana kwa kusimamia Wizara ya Afya, tunakushukuru kwa umahiri wako, taifa hili tunakutegemea,” amesema Bashungwa.

Aidha, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ametoa wito kwa wamiliki wa viwanda vya dawa na vifaa tiba kuzalisha vifaa kinga vya kutosha ili kukabiliana na janga la Corona nchini ili kuondokana na changamoto ya ucheleweshaji wa kupata vifaa kinga kutoka nje ya nchi

“Tukizalisha hapa nchini tutaokoa rasiliamali fedha nyingi, muda pia tutazalisha ajira na kuwa na uhakika wa   ubora na usalama unaohitajika kupitia mamlaka zetu za ndani kwa urahisi”. Alisema Waziri Ummy.

Waziri amesema kuwa bado kuna uhitaji mkubwa wa vifaa kinga , hivyo wale wote wanaozalisha vifaa kinga wanatakiwa kuongeza uzalishaji ili kutosheleza mahitaji ya soko nchini na hata kuweza kuuza nchi za jirani.