Waziri wa Afya wa Tanzania, Ummy Mwalimu amesema kuwa ripoti ya uchunguzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii inaonesha kuwa mashine moja ya kupima sampuli za COVIDー19 ilikuwa na hitilafu, na uongozi wa maabara hiyo haukuchukua hatua za kuifanyia matengenezo kwa wakati.

“Upimaji wa Sampuli zote za Covid-19 umehamishiwa katika maabara Mpya iliyokamilika kujengwa katika eneo la Mabibo Dar es Salaam ambayo kwa sasa ndiyo itakuwa maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii,Maabara hii mpya ina uwezo wa kupima sampuli 1800 za Ugonjwa wa Covid -19 ndani ya masaa 24 tofauti na ile ya awali ilokua na uwezo wa kupima sampuli 300 tu,Mojawapo ya Mashine za kupima sampuli za Covid-19 ilikua na hitilafu bila Uongozi wa Maabara kuchukua hatua za kuifanyia matengenezo kwa wakati” Ummy Mwalimu – Waziri wa Afya

The post Waziri Ummy atoa ripoti ya uchunguzi wa maabara ya kupima corona ‘mashine ilikuwa na tatizo’ appeared first on Bongo5.com.