Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Khamis Kigwangalla ametoa povu dhidi ya waliohusika kumuua mamba huku akiwaita watu hao wana roho mbaya.

Awali ilielezwa kuwa mamba huyo aliuliwa kwa sababu alikuwa anakwenda nchi kavu ili amdake kitoto kichanga.

Kigwangalla baada ya kuona picha hiyo ya kuuliwa kwa mamba aliandika ujumbe katika ukurasa wake wa Twitter.

“Watu wenye roho mbaya kabisa nyie mnamsingizia tu mamba wa watu, kwanza bado mdogo,” aliandika Kigwangalla.

Aliongezea kuwa “Hivi kitoto kichanga kitakaa kwenye kingo za mto peke yake? Kinafanya nini mpaka mamba akimendee? Hivi unajua tabia za mamba za kuwinda zilivyo?,” alihoji waziri.