Waziri wa Maji @jumaa_aweso amezitaka Mamlaka za Maji zote nchini kuanza kutoa Elimu ya Usomaji Mita za Maji kwa wateja wake ili kupunguza malalamiko mengi kutoka kwawateja kuhusu malipo ya ankara za maji.

Amesema hivi sasa kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu kulipia gharama kubwa za maji ukilinganisha na matumizi yao halisi kwa mwezi. “Asilimia kubwa hawajui namna mita zinavyohesabu, jinsi ya kuzisoma na gharama za kila uniti, hivyo basi ni jukumu la mamlaka kuhakikisha wateja wake wanapata elimu hii kila wanapokwenda kusoma mita kwenye nyumba za wateja,” alisema Aweso

Aliongeza “Naamini hatua hii itapunguza malalamiko na itaamsha ari ya wananchi kulipa ankara zao kwa wakati”

Pia alisema kazi ya utekelezaji wa Mradi wa Maji katika Mji wa Chamwino inaendelea vizuri na wiki ijayo tutatoa Sh. milioni 700 kati ya mil 855 kwa ajili ya ujenzi wa tenki la ukubwa wa lita milioni 2.5 na ununuzi wa pampu ili kuharakisha utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mradi.

The post Waziri Jumaa Aweso atoa maagizo wasoma mita za maji wapigwe msasa (Video) appeared first on Bongo5.com.