Maelfu ya Wapalestina kutoka eneo la Ukingo wa Magharibi leo wamevuka mpaka na kuingia Israel kwa lengo la kufanya kazi baada ya wiki kadhaa za kushindwa kufanya hivyo kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.

Msemaji wa wizara ya kazi ya Palestina amesema jumla ya wapalestina 40,000 wamepatiwa vibali vya kuvuka mpaka kati ya Jumapili na kesho Jumatatu, ili kufanya kazi nchini Israel kwa muda wa mwezi mmoja.

Machi 25, Waziri Mkuu wa Palestina Mohammed Shtayyeh aliwarai vibarua walioko Israel kurejea Ukingo wa Magharibi kama sehemu ya juhudi za Palestina za kuzuia kusambaa virusi vya corona kutoka taifa hilo la Kiyahudi.

Wakati huo huo Israel ilikuwa na visa 2,369 ikilinganishwa na visa 62 vilivyorikodiwa upande wa mamlaka ya ndani ya Palestina.

The post Wapalestina waanza kuingia Israel kufanya kazi appeared first on Bongo5.com.