Manchester United wanataka kuongeza mkataba wa mkopo wa mshambuliaji wa Nigeria Odion Ighalo, 30 , kutoka Shanghai Shenhua. (Standard)

Odion Ighalo

Liverpool, Southampton na RB Leipzig wanamuwania winga wa Werder Bremen Milot Rashica, 23, ambaye mkataba wake utakwisha mwezi Juni. (Bild-in German)Layvin Kurzawa

Layvin Kurzawa kutoka Paris St-Germain

Matumaini ya Arsenal ya kumsajili beki wa kushoto Layvin Kurzawa kutoka Paris St-Germain yamezimika , mchezaji huyo atamwaga wino kukipiga katika klabu ya Barcelona. (Le 10 Sport -in French)

Roma inawataka Arsenal walipe sehemu ya mshahara wa pauni 180,000 kwa wiki kwa ajili ya kiungo wa kati Henrikh Mkhitaryan,31 ikiwa timu hiyo ya ligi kuu ya England itataka mkataba wake wa mkopo kuwa wa kudumu. (ESPN)

Manchester United imetoa ofa kwa mshambuliaji Angel Gomes, 19, ya mkataba wa mshahara wa pauni 300,000 kwa wiki, ili kumzuia kuondoka katika kipindi cha majira ya joto na kumhakikishia mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Uingereza kwa wachezaji wa chini ya miaka 20 kuwa yuko kwenye mipango yao ya baadae ingawa klabu hiyo inamtaka kiungo wa kati wa Birmigham City, Jude Bellingham, 16. (Sun)

Angel Gomes

Mshambuliaji Angel Gomes wa Manchester United

Liverpool na Manchester City wanavutiwa na kiungo wa kati Mbelgiji Aster Vranckx,17, anayechezea KV Mechelen.(Mirror)

Manchester City wanaandaa kitita cha pauni milioni 28 kwa ajili ya kumnasa mchezaji wa nafasi ya ulinzi katika klabu ta Marseille Boubacar Kamara,20. (Le 10 Sport-in French)

Washika bunduki wanapendelea kumsajili mchezaji wa RB Leipzig, Dayot Upamecano, 21, kiwapiku Tottenham na Manchester United, ambao pia wanamtomlea macho mchezaji huyo anayecheza nafasi ya ulinzi .(Football.London)Tiemoue Bakayoko won the French title at Monaco

Tiemoue Bakayoko alishinda taji la Ufaransa kwa timu ya Monaco

Kiungo wa Chelsea Tiemoue Bakayoko, ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo Monaco, anataka kurejea AC Milan. Mchezaji huyo, 25, alitumia msimu wa mwaka 2018-2019 kwa kucheza kwa mkopo San Siro. (Calciomercato-in Italian)

Kocha wa Crystal Palace Roy Hodgson, 71 atakuwa tayari kufanya kazi ikiwa ligi kuu itaanza tena, ingawa kumekuwa na hofu kuwa atapaswa kujitenga kwa sababu ya sheria zilizowekwa kwa ajili ya kupambana na virusi vya corona. (Mail)

Mlinda mlango wa Liverpool, Loris Karius,26 anajiandaa kurejea kwenye klabu yake kwa ajili ya kumalizia miaka miwili iliyobaki ya mkataba wake baada ya mkataba wake kuchezea Besiktas kwa mkopo kufutwa. (Fanatik via Sport Witness)

Jurgen Klopp alitupilia mbali nafasi ya kuifundisha Mexico mwaka 2015 ili kuwa kocha wa Liverpool. (Goal)

The post Wanaowaniwa katika dirisha la usajili barani Ulaya hawa hapa appeared first on Bongo5.com.