Mamia ya waandamanaji walikusanyika jijini humo kutaka haki ifanyike baada ya mauaji hayo ambapo polisi mweupe (Mzungu) alingandamiza kwa goti shingoni akiwa amelala chini wakati anakamatwa. ambapo Floyd alikuwa akipiga kelele “Siwezi kupumua” na “Usiniue!”
Kundi kubwa la waandamanaji wa rangi tofauti lilipita mitaani likipiga kelele na kubeba mabango yaliyokuwa yanashutumu mauaji ya watu weusi na kutaka hatua kali zichukuliwe kwa wahusika, hususan polisi.
Baadhi ya mabango waliyokuwa wamebeba waandamanji.
Meya wa jiji la Minneapolis , Jacob Frey, aliomba radhi kwa familia ya Floyd jana na kusema “Floyd hakutakiwa kufa.”