Virusi vya corona vimewaathiri wahudumu wa afya wapatao 10,000 nchini Iran, kulingana na taarifa za vyombo vya habari vya jana Alhamisi zilizomnukuu Naibu Waziri wa Afya Qassem Janbabaei, ambaye hakufafanua zaidi.

Iran says 10,000 of its health workers infected with coronavirus ...

Ripoti za mapema wiki hii, zimesema idadi ya wafanyakazi wa huduma ya afya walioambukizwa virusi hivyo ni 800 tu.

Iran imesema zaidi ya watu 100 miongoni mwa wa wafanyakazi hao wamefariki. Iran ni taifa la Mashariki ya Kati linalokabiliwa na mripuko mbaya zaidi wa virusi vya corona, ambapo takriban watu 7,249 wamepoteza maisha kati ya watu 129,000 waliothibitishwa kuambukizwa virusi hivyo.

Takwimu hizo ni pamoja na vifo zaidi ya 66 vilivyotangazwa jana Alhamisi na msemaji wa Wizara ya Afya Kianoush Jahanpour.

The post Wahudumu wa Afya 10,000 wapata Corona, Iran appeared first on Bongo5.com.