Wizara ya Afya nchini humo imetangaza ongezeko la Wagonjwa wengine 28 na kufanya jumla ya visa vya Corona nchini humo kufikia 281

Wagonjwa 21 ni madereva wa malori walioingia Uganda kupitia mpaka wa Elegu wakitokea Sudan Kusini huku 7 ni waliokuwa Karantini baada ya kukutana na madereva waliotangazwa awali

Kati ya madereva 21, 7 ni raia wa kigeni kutoka Tanzania (4), Congo (1), Burundi (1) na Eritrea (1). Wote wamekabidhiwa kwa nchi zao

Aidha, Wizara hiyo pia imetangaza jumla ya Wagonjwa waliopona kuwa 69. Jumla ya sampuli zilizopimwa jana na kuleta matokeo hayo ni 2,004