Uganda imetangaza visa vipya 24 vya COVID19 vimeongezeka na vyote vikiwa ni vya Madereva wa Malori na kufanya jumla ya visa kufikia 227

Wizara imesema jumla ya sampuli 2,598 zimepimwa kati ya hizo; 2,044 ni za Madereva wa malori na 554 ni za Wakazi wa Uganda ambapo zote 554 zimeonekana hazina maambukizi

Katika visa hivyo 24, Waganda ni 3 na Wakenya 2 ambao hao wamegundulika katika mpaka wa Elegu. Wengine waliogundulika katika mpaka wa Mutukula ni Watanzania 6 na Mganda mmoja. Pia, Wakenya 12 waliogundulika katika mpaka wa Malaba

Lakini pia, Jumla ya Wagonjwa 63 wamepona nchini humo tangu kuzuka kwa janga hilo