Wizara ya Afya Uganda imesema kuna ongezeko la wagonjwa wapya 43 wa corona wote wakiwa ni madereva wa malori na kufanya jumla ya maambukizi kufikia 203 kutoka 160

Miongoni mwa 43 hao 17 ni waganda,14 wakenya,Watanzania 5,raia wa Eriteria 4,raia wa Burundi 2 huku utambulisho wa 1 ukiwa bado haujajulikana.

Sampuli 720 zilizokusanywa kwenye jamii nchini humo hazijaonyesha maambukizi yoyote.

Jumla ya sampuli zilizofanyiwa uchunguzi ni 2558,waliopona wakiwa 63.