Idadi ya wagonjwa wa virusi vya corona Kenya imefikia 1,214, baada ya wagonjwa wapya 22 kuthibitishwa leo Jumapili.

Wakati wa mkutano na vyombo vya habari , katibu tawala wa wizara ya afya nchini Kenya Rashid Aman amesema kwamba wagonjwa hao ni kati ya umri wa miaka 24 hadi 73 ,huku, wanaume wakiwa 17 na wanawake wakiwa watano.

Dkt Aman amesema kwamba wagonjwa watatu wamepona na hivyo basi kufanya idadi ya wagonjwa waliopona virusi hivyo kufikia 383.

Amesema kwamba mgonjwa mmoja ambaye aligunduliwa kuwa na virusi hivyo katika eneo la Mathare amefariki, na kufanya idadi ya waliokufa nchini humo kufikia watu 51.