Kampuni ya Twitter imewaambia wafanyakazi wake kwamba wanaweza kufanyia kazi nyumbani “daima” kama wanataka kufanya hivyo wakati ikitathmini hali ya baadae ya mtandao huo wa kijamii baada ya janga la virusi vya corona.

Twitter logo on a smartphone with a computer model of the Covid-19 coronavirus.

Uamuzi huo umekuja huku kampuni hiyo kubwa ya mtandao wa kijamii ukisema kuwa hatua zake za kufanyia kazi nyumbani wakati wa hamri ya kukaa nyumbani zimekua za mafanikio.

Lakini pia imesema kuwa itawaruhusu wafanyakazi kurejea ofisini iwapo watachagua kufanya hivyo itakapofungua ofisi zake.

Mapema leo asubuhi Google na Facebook zilisema kuwa wafanyakazi wake wanaweza kufanyia kazi nyumbani hadimwishoni mwa mwaka huu.

Twitter imesema: “Miezi michache iliyopita imeonyesha kuwa tunaweza kufanya hiyo kazi. Kwa hiyo kama wafanyakazi wetu wako katika nafasi na hali ambayo inawawezesha kufanyia kazi nyumbani na wanataka kuendelea kufanya hivyo daima, tutawezesha hilo kufanyika .”

Tangazo hilo limeelezewa kama “enzi inayoelezea hali ” na wataalamu wa uvumbuzi wa digitali.

Blogi yaTwitter iliendelea kusema kuwa kwa wale walio makini kurejea katika ofisiza Twitter Twitterhe “wataendelea kukaribishwa kwa moyo mkunjufu, kwa baadhi ya tahadhari za ziada”.

Kampuni hiyo yenye makao yake makuu mjini San Francisco-inawaajiri 4,000 katika ofisi zake zote duniani.

Imewaruhusu wafanyakazi wake kufanya kazi kutoka nyumbani tangu mwezi Machi na haitarajii kufungua tena ofisi zake kabla ya mwezi Septemba.

Sree Sreenivasan, Profesa wa uvumbuzi wa Digitali katika Chuo Kikuu cha Stony Brook cha Uandhishi wa habari, alisema kuwa ni “enzi ya mabadiliko katika era-habari”.

“Baadhi ya watu huenda wasitilie maanani hili kwasababu ni Twitter, lakini tunajifunza mengi kutoka kwa Silicon Valley kuhusu namna unavyoweza kufanya kazi kwa njia mbali mbali . Kumekua na mawazo kwamba kufanyia kazi nyumbani ni kumuibia muajili na kwamba kufanya kazi ana kwa ana ofisini ni muhimu zaidi.

“Lakini watu wanathibitisha kwamba wanaweza kufanya kazi vema na kutekeleza malengo yao ya kikazi wakiwa nyumbani. Watu wengi wananiambia kuwa wanafanya kazi kwa bidii zaidi wakiwa nyumbani na wanachoka ,” aliongeza.

Makampuni katika maeneo mbali mbali duniani wanaangalia jinsi ya kufungua ofisi zao taratibu huku wakianzisha hatua za kutokaribiana.

The post Wafanyakazi Twitter waruhusiwa kufanyia kazi nyumbani daima   appeared first on Bongo5.com.