Newcastle imeanza mazungumzo ya kumsajili kiungo wa kati wa Barcelona Philippe Coutinho, 28, baada ya Bayern Munich kubadili nia ya kumpatia mkataba wa kudumu nyota huyo wa kimataifa wa Brazil. (Mundo Deportivo – in Spanish)

Kiungo wa kati wa Barcelona Philippe Coutinho

Magpies pia wanamlenga kiungo wa kati wa Liverpool Xherdan Shaqiri, 28, dirisha la uhamisho wa wachezaji litakapofunguli tena msimu wa joto. Kiungo huyo wa kimataifa wa Uswizi amewakilisha klabu hiyo mara 10 tu msimu huu. (Mail)Xherdan Shaqiri with a great strikeKiungo wa kati wa Liverpool Xherdan Shakiri

 

Arsenal na Tottenham wanang’ang’ania kumsajili kwa mkataba wa bila malipo kiungo wa kati wa Chelsea na Brazil Willian, 31, ambaye mkataba wake Stamford Bridge unakamilika msimu huu. (Telegraph)

Wolves huenda wakamnunua kiungo wa kati wa Sporting Lisbon Joao Palhinha, 24. (Mirror)Chelsea

Manchester City wanaongoza katika kinyang’anyiro cha kumsaka kinda wa Ajax Sontje Hansen, 18, ambay alishinda tuzo ya Golden Boot katika kipute cha kombe la dunia kwa wachezaji walio na umri wa chini ya miaka 17 msimu uliopita. (Goal)

Klabu ya Vitoria Guimaraes inataka kumnunua mchezaji kinda wa Crystal Palace Jadan Raymond, 16, kwa £250,000 kandarasi yake ikielekea kumalizika mwisho wa mwezi ujao. (Sky Sports)

The post Wachezaji wanaotikisa usajili barani Ulaya na wanaosumbua vichwa vya mabosi wa klabu hawa hapa  appeared first on Bongo5.com.