Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 21 mei 2020 amewaapisha Viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni. Viongozi hao walioapishwa ni 1. Dkt. Godwin Oloyce Mollel kuwa Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wanawake Wazee na Watoto. 2. Dkt. Delphine Diocles Magere kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani. 3. Dkt. Jacob Gideon Kingu kuwa Balozi wa Tanzania nchini Algeria 4. Balozi Mteule Phaustine Martin Kasike kuwa Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji 5. Balozi mteule John Stephen Simbachawene kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya 6. Brig. Gen. John Julius Mbungo kuwa Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU. Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma.

Katika ghafla hiyo rais Mugufuli amesema kuwa kuanzia tarehe 1/06/2020 Vyuo vyote vifunguliwe, vijana waliokuwa kidato cha sita ambao wanajiandaa kwenye mitihani yao, nao kurudi mashuleni huku michezo nayo ianze tena kwa ligi mbalimbali hapa nchini. Wakati ndege za watalii zikianza kuingia nchini kuanzia tarehe 27 na 28 ya mwezi huu wa tano.

 

 

 

 

The post ”Vyuo, michezo ruksa 1/06/2020, watalii kuingia nchini mwezi huu,”- Rais Magufuli (+Video) appeared first on Bongo5.com.