Muda mfupi baada ya Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kuwafuta uanachama wabunge wake wanne, Anthony Komu (Moshi Vijijini), Joseph Selasini (Rombo), David Silinde (Momba) na Willfred Lwakatare (Bukoba Mjini) kutokana na kukiuka miongozo ya chama hicho, Silinde amezungumza  na kutoa tamko lake kuhusu uamuzi huo wa chama chake.

"Kwa mara ya kwanza pamoja ya kwamba nimesikia kwenye vyombo vya habari, kitu ambacho kimenishangaza ni uamuzi wa kitoto wa CHADEMA

"Huwezi kumfukuza mtu ambaye haujamuita, hujampa mashtaka yake maana mambo yote nilipaswa kuelezwa kwamba kosa lako ni hili, kuna utaratibu wa kumhukumu Mbunge, huo utaratibu haujafanywa

"Naisubiri hiyo barua nitaiona na nitazungumza na vyombo vya habari kuhusu mustakabali wangu wa kisiasa.,” amesema Silinde na kuongeza;
  
“Nimekishughulikia hiki chama kwa miaka 10 nikiwa mbunge na mwanachama, mimi bado ni kijana mdogo sana, miaka 35, wameahidi kunishughulikia lakini mimi naahidi pale nilipoweka jasho langu nitahakikisha narudisha. "