Vifo vya corona vinakaribia kufikia Laki moja Marekani ambapo hadi leo asubuhi kuna vifo 99,300, maambukizi pia yanaongezeka 

Marekani ina maambukizi 1,686,436 na wamepona Watu 451,702

Rais Trump jana alionekana akicheza Gofu huku wakazi wa Marekani wakijianika juani wakati hatua za vizuizi zikianza kulegezwa nchini humo. 

Trump ambaye anataka makanisa, masinagogi na misikiti kuruhusiwa haraka kuendesha ibada, hakuwa amevaa barakoa wakati alipokuwa akicheza Gofu, na hata wachezaji wenzake nao hawakuvaa Barakoa.