Idadi ya wagonjwa waliofariki kutokana na virusi vya corona nchini Marekani imefika  102,107 katika kipindi cha chini ya miezi minne.

Taifa hilo limeandikisha vifo vingi zaidi ya taifa lolote lile huku watu 1,745,803  wakithibitishwa kuambukizwa virusi hivyo idadi ambayo ni asilimia 30 ya maambukizi yote duniani.

Maambukizi ya kwanza nchini Marekani yaliripotiwa mjini Washington tarehe 21 mwezi Januari.

Kufikia sasa idadi ya waliofariki nchini Marekani imefikia 102,107, kulingana na Chuo kikuu cha John Hopkins mjini Maryland ,ambacho kimekuwa kikifuatilia mlipuko huo. Waliopona 490,130