Rais wa Marekani Donald Trump ametoa amri jana ya bendera kushushwa nusu mlingoti kwa siku tatu mfululizo, kuomboleza vifo vya Wamarekani waliokufa kutokana na virusi vya corona. 

Trump ameamrisha hatua hiyo, baada ya idadi ya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa COVID-19 kufika  96,363 nchini humo.

 Aidha Trump amesema bendera zitabakia nusu mlingoti Jumatatu ijayo ambayo ni Siku ya Mashujaa nchini humo, kuwakumbuka wale ambao wamepoteza maisha wakilitumikia jeshi la Marekani.

 Ingawa idadi ya vifo vya kila siku nchini humo haikuongezeka, watu bado wanaendelea kupoteza maisha, na hesabu kamili inapindukia vifo  96,363  - likitajwa kuwa ni taifa lenye vifo vingi ulimwenguni.