Jezi mpya za klabu ya Manchester United za nyumbani zinazodhaniwa kuwa ni za msimu ujao wa mwaka 2020/21 zimevuja mtandaoni huku mashabiki wakizisifu kutokana na kuwa na muundo rahisi.
Kulikuwa na hofu kuwa huwenda jezi hizo zikawa ni zile zilizovuja kabla ya hizi ambazo mashabiki wengi walizichukia huku muonekano wake wakizifananisha na siti za basi kupitia akaunti ya mtandao wa Twitter. Lakini mapokezi ya hizi yamekuwa mazuri zaidi kwa mashabiki.
Jezi iliyowachukiza mashabiki wa United na kulinganishwa na siti za basi
Uzi huo wa Mashetani Wekundu uliovuja kupitia mtandao wa ‘Footy Headlines,’ una rangi nyekundu iliyokolea na logo nyeupe ya Adidas.
The post Uzi mpya wa Manchester United msimu wa 2020-21 wavuja mtandaoni appeared first on Bongo5.com.