Manchester United watalazimika kulipa paundi milioni 80 kwa ajili ya kumnasa kiungo mshambuliaji wa klabu ya Aston Villa, Jack Grealish mwenye umri wa miaka 24, hata kama timu yake itashuka daraja msimu huu. (Mirror)

Kikosi cha mastaa waliokiwasha na Mbwana Samatta - Mwanaspoti

United walitarajia kumng’oa nyota huyo ambaye anakipiga na Mtanzania Mbwana Samatta ndani ya klabu hiyo ya Aston Villa inayoshiriki ligi kuu pale England kwa dau la paundi milioni 50, lakini jambo ambalo linaonekana kugonga mwamba.

Kiungo wa kati wa Bayern Munich Corentin Tolisso pia analengwa kusajiliwa na klabu ya Manchester United. Bayern iko tayari kumuza mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa 25 kwa ajili ya kupata fedha ili kununua wachezaji wengine, akiwemo winga wa Manchester City mjerumani Leroy Sane, 24. (Express)

Juventus itakuwa kwenye kinyang’anyiro na Manchester United kumnasa mshambuliaji wa Wolves Raul Jimenez, 29. (Times)Raul Jimenez

Juventus na Man United kuchuana kumnasa Raul Jimenez

Winga wa Bournemouth na Scotland Ryan Fraser,26, anaaminika kuwa anapenda kujiunga na Tottenham kwa uhamisho wa bure punde tu baada ya mkataba wake na kbalu yake ya sasa utakapokamilika tarehe 30 mwezi Juni. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Liverpool Pedro Chirivella,22, amepewa ofa ya mkataba wa miaka mitano lakini hajaamua bado kuhusu mustakabali wake, tayari klabu za Nates na Rangers wameonesha kuwa na nia ya kumchukua. (Goal)Nicolo Zaniolo

Liverpool inafikiria kumsajili mshambuliaji wa Roma Nicolo Zaniolo

Liverpool inafikiria kumsajili mshambuliaji wa Roma Nicolo Zaniolo, 20, ambaye pia analengwa na Manchester United na Tottenham. (Corriere dello Sport – via Sports Mole)

Wakati huohuo, inadaiwa kuwa Liverpool tayari ilishaanza kuchukua hatua kuhusu uhamisho huo muhimu wa Zaniolo kabla hata janga la corona halijaathiri mchezo wa kandanda. (Il Tempo)Diego Llorente

Diego Llorente ananyemelewa na Liverpool na Monaco.

Mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa timu ya Real Sociedad Diego Llorente, 26, anatazamia kuihama klabu yake huku Monaco na Liverpool zikiwa timu zinazomtolea macho. (La Razon)

Crystal Palace wana mpango wa kuwachukua watu watatu kutoka Burnley, kocha Sean Dyche, winga Dwight McNeil,20 na mchezaji wa nafasi ya ulinzi James Tarkowski, 27. (Mirror)Milan Skriniar

Milan Skriniar

Manchester United itapaswa kuipiga kumbo Real Madrid kama watataka kumnyakua, Milan Skriniar, 25, ambaye timu yake ya sasa ya Inter Milan inajiandaa kumruhusu mchezaji huyo kuondoka. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Fiorentina Chriastian Koffi, 19 , aliamua kutojiunga na Liverpool mwaka 2018 lakini anasema hakufanya makosa. (sofoot – in French)

The post United watalazimika kumng’oa swahiba wa Samatta, Aston Villa kwa dau la paundi milioni 80 appeared first on Bongo5.com.