Mkufunzi wa zamani wa the Gunners, Unai Emery anadai kuwa alilazimishwa kumsajili winga Nicolas Pepe, 25, kujiunga na Arsenal – na kufichua kuwa kwa upande wake alimtaka mshambuliaji Wilfried Zaha, 27, baada ya kufanya mazungumzo na nyota huyo wa Crystal Palace. (Mail)

Real Madrid bado wana nia ya kumnunua Erling Braut Haaland na watamfuatilia mshambuliaji huyo wa miaka 19- leo Jumamosi wakati Borussia Dortmund watarejea uwanjani katika ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga. (Mundo Deportivo – in Spanish)

Chelsea wako tayari kuwauza baadhi ya wachezaji wake katika kikosi cha kwanza ili kupata kiungo wa kuimarisha timu yao msimu huu lakini hawana nia ya kupokea ofa ya kuwauza wachezaji N’Golo Kante, 29, na Jorginho, 28. (ESPN)Jesus

Manchester City wanajiandaa kumpatia mshambuliaji wa Brazil Gabriel Jesus mkataba mpya wa thamani ya £120,000 -kwa wiki kuzuia nyota huyo wa miaka 23- asinyakuliwe Juventus. (Sun)Gabriel Jesus

Lakini City wanataka kumuuza kiungo mshambulizi wa kati Leroy Sane msimu huu, licha ya masharti yao makali dhidi ya Bayern Munich kuhusu uhamisho wa Mjerumani huyo wa miaka 24. Mkataba wa Sane unaingia miezi 12 ya mwisho mwisho wa msimu. (Evening Standard)

Kiungo wa kati wa Ujerumani Toni Kroos, 30, amepuuzilia ambali uwezekano wake kuungana tena na Pep Guardiola Manchester City ana amesema kuwa anatarajia kukamilisha taaluma yake ya soka katika klabu ya Real Madrid. (Eurosport)

Sergej Milinkovic -Savic anayenyatiwa na Tottenham Hotspur hana mpango wa kuitikia uhamisho wa lazima kutoka Lazio msimu huu. Mchezaji huyo nyota wa Serbia wa miaka 25 huenda akazawadiwa mkataba mpya wa mwaka mmoja wenye thamani ya £3.5m kwa uaminifu wake kwa klabu hiyo. (Corriere dello Sport via HITC)

Liverpool wako tayari kumnunua mshambuliaji wa miaka 17- Mbrazil Talles Magno. Kinda huyo ambaye usakataji kabumbu wake umelinganishwa Neymar, tayari anacheza katika kikosi cha kwanza cha klabu ya Brazil Vasco da Gama. (Mirror)Valentino LazaroValentino Lazaro

Newcastle wanafanya mazungunzo kuhusu uhamisho wa thamani ya £21.25m ya nyota wa Inter Milan Valentino Lazaro baada ya winga huyo wa Austria kuonesha umahiri wake alipokuwa wakicheza kwa mkopo katika klabu hiyo msimu huu. (Sun)

Wakala wa kiungo wa kati wa Arsenal Lucas Torreira, 24, anadai kuwa mchezaji huyo ana mpango wa kuondoka uga wa Emirates na kurejea Italia. (Tuttomercatoweb via Metro)Nicolas Pepe, 25,Nicolas Pepe, 25

Leicester City hawana mpango wa kumuuza Wilfred Ndidi dirisha la uhamisho la wachezaji litakapofunguliwa licha ya tetesi inayomhusisha kiungo huyo wa kati wa Nigeria wa miaka 23- na mamba wa Ufaransa Paris St-Germain na Manchester United. (All-Nigeria Soccer)

Barcelona wanamsaka kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen Kai Havertz. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 amehusishwa Liverpool lakini Barca wana nafasi ya nzuri ya kumsajili. (Sport1 – in German)

The post Unai Emery : Nililazimishwa kumsajili Nicolas Pepe, Arsenal  appeared first on Bongo5.com.