Rais Yoweri Museveni ametangaza kuwa serikali yake itatoa barakoa za bure kwa wananchi kuanzia miaka sita na kuendelea.

Akihutubia taifa Jumatatu,kiongozi huyo mwenye miaka 75 alisema ni lazima wananchi wote wavalie maski katika maeneo ya umma huku taifa hilo likijiandaa kurejesha uchukuzi wa umma kuanzia Juni.

Rais Yoweri Museveni alisema ni lazima Waganda wote wavalie maski kabla usafiri wa umma kurejeshwa.

“Maski hizi ni lazima zivaliwe kila wakati unatembea maeneo ya umma, endapo unapiga chafya, unazungumza ama kukohoa. Watu walilalamika  hawana uwezo wa kupata maski, serikali imeamua kutoa maski kwa kila Mganda kuanzia miaka sita na kuendelea," alisema Museveni.

Wizara ya Afya nchini humo imesema wagonjwa wengine 12 wa corona wameongezeka na kufanya idadi ya maambukizi kufikia 260, waliopona wamefikia 63 na hakuna kifo