Rais Donald Trump amesema Kikosi Kazi cha Ikulu kinachosimamia janga la #COVID19 kinatarajiwa kuvunjwa na mkakati uliopo hivi sasa ni kufungua uchumi wa nchi hiyo.


Ameongeza kuwa Kikosi hicho kimefanya kazi nzuri hadi sasa lakini Marekani haiwezi ikaendelea kufungwa kwa miaka mitano ijayo, hivyo kinachoangaliwa kwa wakati huu ni usalama na kufungua nchi.

Akitembelea kiwanda cha kutengeneza barakoa kilichopo Arizona, Rais Trump amesema hatua hiyo haimaanishi kila kitu kinaenda sawa, na ni kweli kuna watu waathirika vibaya lakini inapaswa kufungua taifa hilo mapema.

Kwa mujibu wa CNN. Kikosi hicho kiliundwa Januari mwaka huu na Makamu wa Rais, Mike Pence alitajwa kuwa Mwenyekiti. Hata hivyo, Rais amesema wataalamu wawili wa ngazi ya juu, Anthony Fauci na Deborah Birx watabaki kama washauri.

Marekani imeathirika zaidi na mlipuko wa #CoronaVirus kuliko nchi yoyote duniani, ikiripoti visa 1,312,960 na vifo 74,429 huku waliopona wakiwa 184,220.

The post Trump kuvunja kamati ya kuhangaika na Corona, Kuhamishia nguvu kujenga Uchumi appeared first on Bongo5.com.