UHUSIANO kati ya Marekani  na China umeendelea kuzorota kwa kasi  tangu kuanza kwa jana la Corona lililoua makumi ya Raia wa Marekani

Jana Mei 14, 2020 , Rais wa Marekani Donald Trump  alisema kwa sasa hana mpango na hataki  kuzungumza na Rais Xi Jinping wa China  na akaenda mbali zaidi na  kusema anafikiria kusitisha uhusiano na taifa hilo la pili kwa nguvu za uchumi duniani. 

Akizungumza na kituo cha televisheni cha Fox, hapo Jana, Trump alisema amesononeshwa sana na kitendo cha China kushindwa kulidhibiti janga la corona. 

Takwimu zinaonesha Marekani imeathiriwa vibaya zaidi na virusi vya corona  kuliko nchi nyingine yoyote Duniani.

Kwa takwimu za leo asubuhi, Maambukizi  ya Virusi vya Corona  nchini humo yamefika 1,457,593, waliopona ni 318,027 tu na vifo vimefika 86,912