Rais Donald Trump wa Marekani amesema serikali yake itawekeza kwa makampuni yote makubwa yanayofanya jitihada za kutafuta chanjo ya virusi vya corona na kwamba imepunguza idadi ya makampuni hayo hadi kufikia 14, huku akitoa ahadi ya kuyapunguza zaidi.

Katika mkutano wake uliofanyikia Ikulu ya Marekani, ambapo ulihudhuriwa na maafisa wengi wa Ikulu hiyo wakiwa wamevaa barakoa, lakini yeye akiwa hajavaa, Trump alionesha matumaiini kwamba kinga ya maradhi ya COVID-19 kabla ya kumalizika mwaka huu.

Na kuongeza kusema serikali yake itashiriki vyema katika usambazaji wa chanjo hiyo pale tu, itakapopatikana.

Hayo yanajiri wakati takwimu mpya zilizotolewa na chuo kikuu cha John Hopkins zinaonesha vifo vipya 1,680 ndani ya kipindi cha masaa 24 yaliopita.

The post Trump: Chanjo ya Corona kupatikana kabla ya kumalizika mwaka 2020 appeared first on Bongo5.com.