Rais Donald Trump wa Marekani amesema anatumia dawa ya hydroxychloroquine ya kutibu Malaria, kujilinda na maambukizi ya virusi vya corona. 

Trump anatumia dawa hiyo licha ya onyo kutoka kwa serikali yake kwamba inatakiwa kutolewa tu kwa wagonjwa wa COVID-19 waliolazwa hospitalini ama kufanyiwa uchunguzi kutokana na uwezekano wa athari mbaya za dawa hiyo. 

Trump amewaambia waandishi wa habari kwamba amekuwa akitumia dawa hiyo pamoja na vidonge vya madini ya zinki kila siku, kwa muda wa wiki moja na nusu sasa. 

Dawa hiyo hata hivyo inasemekana kuwa na athari kwa baadhi ya wagonjwa na haijaonyesha kuwa na uwezo wa kukabiliana na virusi vya corona.

 Trump amesema daktari wake hakumuandikia dawa hiyo, lakini alimuomba daktari wa ikulu ya White House kumuandikia na kusema anaitumia kwa sababu anaamini ni dawa nzuri. 

Rais huyo amekuwa akishinikiza matumizi ya dawa hiyo, ingawa bado hakuna utafiti mpana uliofanyika kuhusiana na uwezo wake katika kutibu COVID-19.

Credit-DW