Rais Donald Trump wa Marekani ameonyesha furaha yake na kupongeza kujitokeza tena hadharani kwa Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un baada ya wiki kadhaa za uvumi kuhusu afya yake.
Vyombo vya habari vya Korea Kaskazini jana vilisema Kim alijitokeza katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha mbolea.
Kim alionekana kwenye picha akitabasamu na kuzungumza na wasaidizi wake katika hafla hiyo na pia kuzuru kiwanda hicho.
Ukweli wa picha hizo haujaweza kubainika lakini inaaminika video hiyo ni ya Ijumaa.
Trump aliandika kwenye ukurasa wa Twitter kuwa anafuraha kumuona tena Kim.
Uvumi kuhusu kifo cha kiongozi huyo ulianzia Aprili 15 pale alipokosa kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa kwa babu yake mwasisi wa taifa hilo siku ambayo ni muhimu sana katika historia ya taifa hilo la Korea ya Kaskazini.
The post Trump apongeza kujitokeza kwa Kim Jong Un appeared first on Bongo5.com.