lucas
Bayern Munich iko tayari kumtoa mchezaji wake mlinzi Lucas Hernandez, 24, kwa Manchester City wakati inapoendelea na azma yake ya kumuwinda winga wa Ujerumani, 24, Leroy Sane. (TZ - via Manchest5r Evening News)
Mauro%2BIcardi
Mshambuliaji wa Argentina Mauro Icardi, 27, anatarajiwa kwamba uhamisho wake hadi Paris St-Germain utakuwa wa kudumu baada ya kufikiwa kwa makubaliano ya £51.2m na Inter Milan. (Sky Sports)
Vincent%2BKompany%252C
Aliyekuwa nahodha wa Manchester City Vincent Kompany, 34, amekataa fursa ya kurejea katika klabu hiyo kama msaidizi wa kocha Pep Guardiola muda mfupi baada ya kuondoka ili kutimiza ndoto yake ya kuwa kocha wa Anderlecht. (Sun)
Alexis%2BSanchez
Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer bado anaweza kuachana na mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez msimu huu huku Inter Milan ikifikiria kuongeza mkataba wake wa makubaliano ya mkopo. (Express)