Mwanamuziki mkongwe wa Bendi ya Kilimanjaro maarufu kama wana njenje, Mabrouk Hamis Omar almaarufu kama Babu Njenje amefariki dunia leo jijini Dar es salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Mmoja wa wanamuziki wa bendi hiyo, John Kitime amesema "Ni kweli Babu Njenje amefariki na sasa naelekea pale alipokuwa akiishi, Mtaa wa Mindu Upanga ambapo taratibu zitafanyika".

 Babu Njenje atakumbukwa kwa nyimbo zake nyingi zikiwemo Njenje, Kinyaunyau na nyingine nyingi.