mwanamuziki mkongwe wa Bendi ya Kilimanjaro maarufu kama Wana-Njenje, Mabrouk Hamis Omar almaarufu kama Babu Njenje amefariki dunia leo jijini Dar baada ya kuugua kwa muda mrefu.

ambaye alizaliwa mwaka 1947 Wilayani Pangani, Tanga.
Marehemu Babu Njenje alianza kazi ya Muziki wakati anasoma shule ya Usagara Sekondari Mkoani Tanga, na baadaye akajiunga na Band ya Love Burg huko Tanga, kisha Marehemu alijunga na Band ya Revolution na ilipofika mwaka 1989 yeye pamoja na wanamuziki wenzake akiwemo Abdallah Dulla,Hemed Salim Chuki, Babu Njenje, Mohamed Mrisho, Waziri Ally pamoja Keppy Kiombile walianzisha The Kilimanjaro Band.

Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) limethibitisha.

The post TANZIA: Babu Njenje afariki dunia, fahamu historia yake appeared first on Bongo5.com.