Mahakama ya juu nchini Marekani imeiamuru Sudani kuwalipa fidia baadhi ya waathiriwa wa shambulio la mabomu mwaka 1998 katika balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania liliotekelezwa na wapiganaji wa kundi la al-Qaeda.

Zaidi ya watu 200 walifariki na maelfu kuathiriwa katika mashambulio hayo.

Sudan ilishutumiwa kwa kuipatia al-Qaeda na Osama Bin Laden usaidizi wa kiufundi na ule wa kifedha.

Uamuzi huo wa mahakama ya juu unawahusha raia wa Marekani, wafanyakazi wa balozi hizo na wanakandarasi.

Uamuzi huo unajiri wakati ambapo serikali ya Sudani inapigania kuondolewa katika orodha ya Marekani ya mataifa yanayofadhili ugaidi.

Sudan ‘yakana kuhusishwa na ugaidi’

Uamuzi huo ulioungwa mkono na majaji wengi unamaanisha kwamba takriban $800m kati ya $4bn ambazo ziliamrishwa na mahakama hiyo kuwafidia mwaka 2011 zimerejeshwa , Christopher Curran, ambaye alikuwa anaiwakilisha Sudan amenukuliwa na Ruters akisema.

Kuna jengo la kumbukumbu katika mji kuu wa Kenya NairobiKuna jengo la kumbukumbu katika mji kuu wa Kenya Nairobi

Miaka tisa iliopita, jaji wa mahakama ya kijimbo mjin Washington alisema kwamba Sudan inafaa kulipa takriban $6bn kama fidia $4bn kama adhabu ya makosa , lilisema gazeti la The New York Times.

Mwaka 2017 , Sudan ilifanikiwa kuupinga uamuzi huo ikihoji kwamba walipatiwa fidia hiyo chini ya marekebisho ya sheria ya 2008 ambayo haiwezi kusimamia kitu kilichotokea miaka 20 iliopita.

Mahakama ya juu iliamua siku ya Jumatatu kwamba bunge la Congress lilisema ilikuwa inawezekana kutumiwa.

Kama kawaida , Sudan iliwaonea huruma waathiriwa wa ugaidi, lakini ikasisitiza kwamba haikuhusika na makosa yoyote yaliofanyika kuhusiana na kitendo hicho, alisema bwana Curran.

Kesi ya kutoa adhabu kwa Wakenya na raia wengine ambao hawakuajiriwa moja kwa moja na ubalozi pamoja na jamaa wa familia zisozotoka Marekani naa wale waliopata majeruhi ama kuuawa katika mashambulio hayo walirudishwa katika mahakama ndogo.

Mathew McGill ambaye alikuwa anawakilisha waathiriwa , alisema: Tuna matumaini kwamba hatua hiyo itasaidia Sudan kuafikia siluhu ya haki kwa waathiriwa wote.

Dola bilioni 6 za kulipa fidia hazikuwa na mgogoro wowote katika kesi hiyo na mwezi Februari iliripotiwa kwamba Sudan ilikuwa katika mazungumzo kuhusu kitita hicho ili kulipwa.

Wakati huo Sudan ilikuwa imekubali kuzifidia familia 17 za wanamaji walofariki wakati meli yao USS Cole iliposhambuliwa na al-Qaeda katika bandari ya Yemen 2000.

Haya yalikuwa masharti muhimu yaliowekwa na Marekani kwa Sudan kuondolewa katika orodha ya mataifa mabaya suala ambalo lingeruhusu vikwazo kuondolewa.

Serikali mpya nchini Sudan iliochukua madaraka kufuatia kupinduliwa kwa rais wa muda mrefu Omar el Bashir iko tayari kuimarisha uhusiano na Marekani hatua ambayo itasaidia kuifanya nchi hiyo kuondolewa vikwazo na kumaliza kutengwa kwa uchumi wake.

Bashir ambaye kwa sasa yuko kizuizini baada ya kuhukumiwa kwa ufisadi alikuwa madarakani wakati balozi hizo na meli ziliposhambuliwa.

The post Sudan kuwalipa fidia waathiriwa na mlipuko wa ugaidi balozi za Marekani Tanzania na Kenya appeared first on Bongo5.com.