Na Zainab Nyamka, Globu ya jamii
DROO ya upangaji wa mechi za robo faini ha Kombe la Azam Sports Federation Cup imefanyika kwa vigogo viwili vya soka kukutana katika hatua hiyo.

Upangaji huo umerushwa moja kwa moja na kituo cha Azam na kusimamiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF).

Katika mchezo wa kwanza, Simba Watakutana na Azam ikiaminiwa ni kuwa mchezo wenye ushindani mkubwa sana kutokana na historia ya mchezo wa ligi uliopita.

Mchezo wa pili utakuwa ni Yanga wakiwakaribisha Kagera katika Jiji la Dar es Salaam, Yanga wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wao wa Ligi na wa kwanza kwa Kocha Luc Eymael wakifungwa goli 3-0 kwenye Uwanja wa Uhuru.

Mchezo wa tatu ni Namungo dhidi ya Alliance ya Jijini Mwanza huku Sahare All Stars timu pekee ya Ligi daraja la kwanza kuingia hatua ya robo fainali wakiwakaribisha Ndanda katika Uwanja wa Mkwakwani Tanga.