Akiongea C.E.O wa klabu hiyo @football_senzo pamoja na msemaji wa klabu hiyo @hajismanara wametolea ufafanuzi juu ya Website hiyo ya Simba ambayo utakuta historia ya klabu hiyo tangu kuanzishwa kwake na Matokeo ya michezo yote ambayo Simba imewahi kucheza, kwa maana nyingine taarifa zote za klabu hiyo tena kwa lugha mbili KISWAHILI na KIINGEREZA.

Mbali na hilo C.E.O bwana @football_senzo amesema kuwa kuna taarifa nyingi sana na amekuwa akipokea simu nyingi za mawakala kuhusu usajili mpya na kusema kuwa lengo lao kwa sasa ni kupeleka nguvu zao kwenye ligi wahakikishe wanashinda taji hilo kwani wapo kileleni mwa ligi lakini pia kupelekea macho na nguvu zao kwenye ligi ya AZAM FEDERATION na kuhakikisha wanafanya vizuri na baada ya hayo yote basi taarifa na wachezaji waliosajili watatangazwa rasmi.

 

The post Simba yafungua website yao rasmi, Manara na Senzo wafunguka wachezaji waliosajili pia mazoezi ya timu kuanza rasmi siku hii – Video appeared first on Bongo5.com.