Mara ya kwanza ilionekana kama picha nzuri iliyotumwa kwenye ukurasa wa Twitter kuwachangamsha watu katika nyakati hizi za corona.

Lakini wakati ilipogundulika kuwa mwanamume huyo aliyeshirikisha umma picha ya binti yake mwenye umri wa miezi 10 akiwa amefungwa mgogoni mwake wakati wa kikao kilichofanyika kwa njia ya mtandao alikuwa ni waziri wa elimu wa Sierra Leone, gumzo liligeuka kuwa la majukumu ya kijinsia.

David Moinina Sengeh alisema kuwa alitaka kutoa mfano kwa wanaume wengine.

Ameiambia BBC kuwa ni nadra sana kumuona mtoto kwenye mgongo wa baba katika nchi yake.

Bila shaka, picha ya mwanamke mwenye mtoto mgongoni haijawahi kuwa kitu cha kushangaza jambo ambalo waziri huyo mwenye umri wa miaka 33 anaafiki.

Kufanya mambo zaidi ya moja wakati wa kikaocha intanet kwa mfumo wa Zoom

“Wanawake wengi hufanya hili kila siku, lakini ni jambo la kawaida sana kiasi kwamba hatulizungumzii kabisa. Kama angelikua ni mke wangu aliyefanya hivyo Twitter hii isingezungumziwa kabisa ,” aliiambia BBC kutoka mji mkuu wa Sierra Leone, Freetown, ambako raia wameambiwa wakae nyumbani lakini bila masharti makali.

Waziri wa elimu alikua jikoni nyumbani akimlisha mwanae Peynina alipoanza kushiriki katika kikao cha video kupitia programu ya intaneti ya Zoom. Alibaini kuwa alikua anaonekana mwenye usingizi, kwa hiyo akaamua kumbeba mgongoni ili kuendelea na mkutano wa kazi.

Presentational white space

Picha hii “iliwalazimisha kujifikia, inawaonyesha kwamba inawezekana kuwalea watoto wao “, Dkt Sengeh alisema.

“Nina marafiki ambao hawajawahi hata mara moja kuwabadilishia nepi watoto wao, na hata hawaelewi ni vipi hilo linawezekana,” aliongeza.

Baadhi ya wanaume walijibu kupitia twitter kwa picha zao wakionyesha juhudi zao za kuwalea watoto wao.

Mfano wa kuigwa

Pia amekuwa akipongezwa na baadhi ya wanaharakati.

“Ni mfano wa kuigwa kwa wanaume wengine nchini Sierra Leone na katika Afrika nzima,” mwanaharakati wa haki za wanawake nchini Sierra Leonean women Nemata Majeks-Walker aliiambia BBC.

“Ni mtu ambaye haamini kwamba ni mwanamke pekee ambaye anapaswa kuwalea watoto.”

Waziri wa elimu pia alitaka kuwatia hamasa viongozi, hususan wanaume wenzake, kushirikisha umma maisha ya familia zao.

Anadhani kwamba imemsaidia kuelewa na kuwahurumia wazazi wengine na itawezesha kuandaa sera bora.

David SengeyHaki miliki ya pichaTED
Image captionKabla ya kuwa waziri wa elimu, Dkt Sengheh alisaidia kutengeneza miguu bandia kwa ajili ya walemavu

Shirka la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu linasema kwamba ” ukosefu wa udawa wa jinsia na kuwanyima wanawake haki zao ni mambo ambayo bado yanashuhudiwa katika jamii ya Sierra Leone “. Tathmini ambayo Dkt anakubaliana nayo.

Amesemakuwa wasichana wengi kuliko wavulana hukatisha masomo kabla ya kumaliza shule za sekondari na anaandaasera, ambazo alizielezea kama “zinazowajumuisha vikali “, ambazo lazima zitainua idadi ya wasichana wanaokaa shuleni.

Mwezi mmoja uliopita, alihusika katika kuondoa marufuku ya kutowarusu wasichana wenye ujaouzito kuendelea na masomo iliyowekwa nchini humo.

Sierra Leone ina visa 124 vya corona vilivyothibitishwa na imekwisharekodi vifo saba kutokana na janga la virusi vya corona.

The post Sierra Leone: Waziri aendesha kikao akiwa na mtoto mgongoni appeared first on Bongo5.com.