Ujerumani inaelekea taratibu kurejea katika hali yamaisha ya kawaida. Shule na biashara kadhaa zitaanza kufunguliwa tena baadae leo katika hatua ya kulegezwa zaidi sheria ya kubaki majumbani iliyowekwa na serikali.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Deutsche Welle (DW), Ujerumani ilitangaza hapo jana Jumapili kufunguliwa tena nyumba za ibada. Wakati huo huo maduka ya vinyozi na saluni pia zinatarajiwa kufungua milango yake baada ya kufungwa kwa karibu miezi miwili.

Ujerumani imeorodhesha idadi ya chini ya maambukizi mapya na pia idadi ya watu waliokufa kutokana na COVID -19 tangu Machi 31.

Idadi ya watu walioambukizwa kote ulimwenguni sasa imepindukia milioni 3.5 wakati watu waliokufa kutokana na janga la corona wanakaribia laki mbili na nusu.

The post Shule na biashara kufunguliwa Ujerumani appeared first on Bongo5.com.