Shirika la hali ya hewa duniani WMO, limesema sehemu ya kaskazini ya dunia sambamba na kanda za kitropiki inatarajiwa kukumbana na joto kali kuliko kiwango cha wastani, katika kipindi cha mwezi huu wa Mei na Juni kwasababu ya ongezeko la joto baharini.

Kulingana na shirika hilo la Umoja wa Mataifa, miezi minne ya kwanza ya mwaka huu imerikodi kila mmoja joto kali zaidi au ya ya pili kwa joto kali zaidi katika rekodi.

Katibu Mkuu wa WMO, Petteri Taalas amesema joto la angani na baharini limeongezeka kwasababu ya mabadiliko ya hali ya hewa na kuleta athari kubwa ya majanga kama vimbunga vya kitropiki na mifumo ya mvua.

WMO inatarajia mvua za juu ya wastani katika bahari ya Hindi, Australia na sehemu ya magharibi ya visiwa vya Indonesia katika miezi ijayo.

The post Shirika la hali ya hewa duniani: Sehemu ya Kaskazini ya Dunia kukumbana na joto kali appeared first on Bongo5.com.