Virusi vya corona huenda ”visiishe”limeonya Shirika la Afya Duniani(WHO), Akizungumza katika kikao Jumatano, Mkurugenzi wa dharura wa WHO, Dkt Mike Ryan ameonya dhidi ya kujaribu kubashiri ni lini virusi vya corona vitatoweka.
Aliongeza kuwa kama chanjo itapatikana, kudhibiti virusi kutahitaji”juhudi kubwa”,
Takribani watu 300,000 kote duniani wameripotiwa kufa kutokana na virusi vya corona, na zaidi ya visa milioni 4.3 vimerekodiwa.
“Ni muhimu kufahamu hili: Virusi vinaweza kuwa janga jingine katika jamii zetu, na , na virusi hivi huenda visiishe ,” Dkt Ryan aliwaambia waandishi wa habari kwa njia ya video kutoka Geneva.
“Virusi vya HIV havijaisha – lakini tumevizowea.”
Dkt Ryan amesema pia kwamba haamini “mtu yeyote anaweza kubashiri ni lini ugonjwa huu utatoweka “.
Kwa sasa kuna chanjo zaidi ya 100 zainazofanyiwa utafiti- lakini Dkt Ryan amesema kuna magonjwa mengine, kama vile tetekuwanga, ambayo bado hayajatokomezwa licha ya kuwa kuna chanjo yake.
Mkurugenzi Mku wa Tedros Adhanom Ghebreyesus alisisistiza kuwa bado inawezekana kudhibiti virusi vya corona, kwa juhudi.
“Suluhu liko mikononi mwetu, na ni shughuli ya kila mtu, na sote tunapaswa kuchangia kuzuia janga hili ,” alisema.
Mtaalamu wa WHO wa majanga Maria van Kerkhove pia ameuambia mkutano wa waandishi wa habari : “Tunapaswa kuweka akilini kwamba itachukua muda kuondokana na janga hili .”
Kauli zao zinakuja huku nchi mbalimbali zikianza kulegeza hatua za kukaa nyumbani, na viongozi wanaangalia uwezekano wa lini na ni vipi wanaweza kufungua shughuli za kiuchumi katika nchi zao.
Dkt Tedros anaonya kuwa hakuna hakikisho juu ya njia za kulegeza hatua za kukaa nyumbani bila kusababisha wimbi jingine la maambukizi.
“Nchi nyingi zingependa kuacha hatua tofauti za kukabiliana na virusi ,” alisema mkuu wa WHO . “Lakini pendekezo letu ni kwamba kukaa chonjo kunahitajika bado katika kila nchi kwa kiwangio kiwezekanacho .”
Dkt aliongeza kuwa : ” Kuna fikra za ajabu zinazoendelea kwamba sheria ya kukaa nyumbani inasaidia kabisa na kwamba kuondolewa kwake kutakuwa vizuri. Yote yanaweza kusababisha hatari .”
The post Shirika la Afya Duniani “Virusi vya Corona vitaendelea kuwepo kama vilivyo virusi vya Ukimwi” appeared first on Bongo5.com.