Ligi Kuu nchini Uingereza ikiwa inatarajiwa kuanza katia ya Juni 12 au 19 huku zikiwa zimesalia mechi 92 ligi hiyo kumalizia msimu wa 2019/20 kuna uwezekano wa kuanza kuoneshwa Live kupitia YouTube bure.

Inatarajiwa kuwa msimu wa 2019-20 bado unaweza kumaliza katika mpangilio huo katika majira ya joto kwa kuchezwa ndani ya wiki saba.

Lakini pamoja na michezo hiyo ikitarajiwa kuchezwa mbele ya viwanja visivyo na mashabiki, bado wakubwa wa mpira wa miguu nchini humo wanataka mashabiki wao waweze kutazama kila mchezo wa moja kwa moja huku wakiwa nyumbani kwa kuepuka misongamano itakayowaepusha na maambukizi ya Corona.

Katika mpango huo uliombwa na maboss wa vilabu vya EPL michezo inatarajiwa  kuoneshwa na Sky Sports, BT Sports na YouTube.

Lakini mara ya mwisho Ligi Kuu ilionyesha mechi za bure ilikuwa siku ya ufunguzi wa msimu wa 2013-14.

Siku hiyo, Sky Sports ilionyesha mchezo kati ya Manchester United dhidi ya Swansea wakati BT Sport iliruhusu mtanange kati ya Crystal Palace vs Arsenal bure.

 

The post Sababu za ligi kuu Uingereza kuonyeshwa bure kwenye mtandao wa Youtube appeared first on Bongo5.com.