“Nakusikiliza upo tayari tukuandike wewe ndio msimamizi wa mgonjwa huyu”
Magreth akamtazama daktari Mkama kisha akamuitikia kwa kutingisha kichwa, akimaanisha kwamba ame kubaliana nahilo.
“Sawa nitakuandikia garama zote hapa ambazo tumeweze kuzitumia katika kumuhudumia mgonjwa wako. Na tutakupigia bei ya yeye kulala ICU kwa siku moja”
“Sawa dokta”
Magreth akakaa kimya huku akimtazama dokta Mkama jinsi anavyo endelea kucharaza kwa peni karatasi iliyopo mezani mwake. Dokta Mkama alivyo maliza kuiandika karatasi hiyo, akaipitia kwa kuisoma kama kila alicho kiandika ni sahihi kisha akamkabishi Magreth. Taratibu Magreth akatupia macho yake kwenye karatasi hiyo. Moyo ukampasuka, kwani garama iliyo andikwa kwenye karatasi hiyo ni kubwa na toka kuzaliwa kwake hajawahi kumiliki kiasi hicho cha pesa.
ENDELEA
“Laki nane dokta….!!!?”
Magreth alishangaa sana huku mikono yake iliyo ishika karatasi hiyo ikimtetemeka kisawa sawa. Akamtazama dokta Mkama kwa mara nyingine, hakuamini kwamba mikono ya daktari huyo ndio aimeandika kiwango hicho kikubwa cha pesa.
“Ndio ni lakini nane. Laiti kama mgonjwa wako angekuwa na bima basi gharama hapo zingepungua”
“Na hii pesa inahitaji ndani ya muda gani?”
“Ndani ya siku mbili hizi la sivyo mgonjwa wako tuta kukabidhi na hato endelea kupata huduma kwenye hospitali hii.”
Maneno ya dokta Mkama yakazidi kumtisha Magreth. Akanyanyuka taratibu huku uso wake ukiwa umepoteza furaha na matumaini. Kila alipo jaribu kutafakari ni wapi ataipata pesa hiyo, akakosa kabisa jibu. Moja kwa moja akarudi nyumbani kwake huku leo ikiwa ni siku mbaya sana kwenye maisha yake.
“Ehee Mungu nitafanya nini ikiwa sina kiasi hichi cha pesa?”
Magreth aliwaza huku akitazama karatasi hiyo ambayo imemkosesha amani kabisa. Taratibu akapiga magoti chini, akachukua biblia yake iliyopo katika kitanda chake cha tano kwa sita. Akaanza kusali huku machozi yakibubujika usoni mwake. Hadi ana maliza kusali maombi ya kumuomba Mungu ampe njia ya kuweza kupata pesa hiyo, aka mkumbuka nabii Sanga, ambaye ni kiongozi wa kiroho katika kanisa analo sali liitwalo HAVEN LIGHT MINISTRY. Magreth akakumbuka juu ya ukaribu wake na mchungaji huyo. Kwajinsi anavyo jitoa katika huduma za kanisani hapo kidogo akapata matumaini ya kuweza kupata msaada wa kiwango hicho cha pesa.
‘Atanisaidia tu’
Magreth alizugumza huku akinyanyuka chini. Akafungua begi lake la nguo na kutoa gauni ambalo kwa mara nyingi hulitumia kuenda nalo kanisani huko. Akamimina maji nusu kwenye kindoo chake cha bafuni na kutoka chumbani kwake kwa haraka.
“Wee weee Mage Mage”
Sauti ya mama mwenye nyumba ikamsimamisha Magreth kwneye kordo hii huku mapigo yake ya moyo yakipoteza matumaini mengine kwani siku zote amekuwa akimkwepa kwepa mwana mama huyo kutokana na
deni la kodi anayo daiwa. Taratibu Magreth akageuka na kumtazama mwana mama huyo.
“Ehee siku hizi nakuona wewe ndio umekuwa mama mwenye nyumba si ndio?”
“Hapana mama shikamoo”
“Shikamoo yako ingekuwa ni pesa basi nina imani kwamba ningekuwa tajiri. Sikuzote unajifanya kutoka alfajiri na kurudi usiku ili usinipe pesa yangu. Sasa ninataka pesa yangu la sivyo nitakufukuza humu ndani”
Bi Ngedere alizungumza kwa jazba huku akifunga tenge lake vizuri. Hakika mwana mama huyu karibia wapangaji wake wote wana muogopa, hii ni kutokana na mdomo wake ulio jaa maneno machafu na usiombee akiwa ana kudai.
“Mama ninakuomba unipe japo siku mbili hizi nitakupatia pesa yako”
“Mwana haramu wewe, huna hata haya. Mama nipe japo siku mbili. Hivi ulikuwepo nilivyo kuwa nina fi** na mume wa mtu hadi kunihonga nyumba eheee?”
“Hapana mama”
“Nilifi** ndio nikajegengwa hii nyumba. Sasa kama na wewe umeshindwa kulipa kodi humu ndani kwangu, nenda kampe mwanaume akujengee ya kwako. Mwana hizaya huoni hata haya. Unajifanya mlokole, mlokole wa mav**. Sasa usipo nipatia pesa yangu leo, haki ya Mungu naapa kesho alfajiri nina kuja kukutolea vitu vyako nje na tuone utafanya nini”
Bi Ngedere mara baada ya kuzungumza maneno hayo, akaachia msonyo mkali na kuanza kurudi chumbani kwake.
“Na nyinyi munachungulia chungulia nini, muniandalie pesa zangu la sivyo na nyinyi yatawakuta ya huyu mwana hidhaya”
Bi Ngedere aliwaambia wamama wawili walio kuwa wakichungulia tukio la mpangaji mwenzao kuchambwa na mwana mama huyo. Magreth huku akiwa amefadhahika, taratibu akanyanyua kindoo chake na kuanza kutembea kwa hatua za wasiwasi na kuelekea katika choo ambacho kwa juu hakijaezekwa na jina maarufu la vyoo hivi huitwa passport toilet.
Magreth akaanza kuoga huku maneno ya bi Ngedere yakiendelea kumtesa kichwani mwake. Akamaliza na kurudi chumbani kwake. Akavaa gauni hilo na kuainza safari ya kuelekea kanisani. Hakuweza kuwasiliana na nabii Sanga kwa maana vijana walio mvamia, waliondoka na pesa zake pamoja na kasimu kake ka tochi. Akafika kanisani hapo majira ya saa kumi na mbili jioni. Akakuta nabii Sanga akiwa na mazungumzo na mama mmoja ambaye naye ni muumini wa kanisa hilo.
“Mage nisubirie hapo nje kwa dakika kadhaa”
“Sawa baba”
Magreth aliitikia kwa unyenyekevu na kukaa eneo la nje ya ofisi hii ya mchungaji anaye muamini kwenye swala zima la kiroho. Hadi ina timu saa moja, mwana mama huyo akatoka huku usoni mwake macho yakiwa ni mekundu na anaonekana ame toka kulia muda si mrefu.
“Mage ingia”
Magreth akasimama na kuingia ndani ya ofisi hii, ambayo imetawaliwa na vitu vya thamani ya juu sana. Ofisi hii ya mchungaji ina hadhi kama ofisi ya raisi.
“Karibu ukae”
Nabii Sanga alizungumza huku akinyanyuka kwenye kiti chake cha kuzunguka, akamuonyesha Magreth aneo lenye sofa za garama na kwa pamoja wakaketi. Nabii Sanga akakunja nne huku akimtazama Magreth usoni mwake.
“Mwanangu una onekana kujawa na mawazo. Kuna tatizo lolote?”
“Ndio baba mchungaji nina matatizo makubwa sana”
Magreth alizungumza huku akivikunja kunja vidole vya mikononi mwake na uso wake akiwa ameuinamisha chini kwa aibu.
“Ohoo pole sana mwanangu. Ehee hembu nieleze ni nini unahitaji nikusaidie mwanangu”
Magreth huku machozi yakimwagika, akaanza kusimulia jinsi siku yake ilivyo kumbwa na matatizo makubwa sana. Hadi ana maliza, nabii Sanga naye alijikuta akilengwa lengwa na machozi.
“Pole sana mwanangu. Sasa fanya hivi, twende hapo Mwananyamala nikamuone huyo kijana kisha nitakupatia pesa ukamlipe huyo mama”
Magreth akalipuka kwa furaha, akamfwata nabii Sanga na kupiga magoti huku akimshika miguu yake.
“Asante, asante sana baba”
Magreth alizungumza huku akiibusu miguu ya Nabii Sanga. Macho ya nabii Sanga yakashindwa kujizuia kutua kifuani mwa Magreth. Kitendo hicho cha kuinama kimeyafanya maziwa ya Magreth yaliyo jaa na kunona, kuonekana kwa asilimia hamsini.
‘Weee shetani niondokee’
Nabii Sanga alizungumza kimoyo moyo huku akimnyanyua Magreth hapa chini. Magreth kwa kuchanganyikiwa akajikuta akimkumbatia mchungaji huyo, ikiwa ndio mara yake ya kwanza kumkumbatia mwanaume maishani mwake. Kwajinsi maziwa ya Magreth yanavyo mchoma choma nabii Sanga kifuani mwake, hakika yakasababisha akili ya nabii Sanga kuhama kabisa. Akajikuta naye akiupitisha mkono wake wa kulia kiunoni mwa Mageth na kuanza kukiminya minya. Kutokana na furaha ya kutatuliwa matatizo yake, Magreth wala hakuhisi kwamba hisia za nabii Sanga tayari zimesha hama.
“Nashukuru sana baba yangu. Mungu azidi kukufunilia na kupata waumini wengi na wengi na ninakuapia, haki ya Mungu nita hakikisha kwamba nita endelea kualika rafiki zangu kuja kusali hapa kanisani kwako”
Magreth alizungumza huku akimuachia nabii Sanga.
“Nashukuru kusikia hivyo mwanangu. Niletee lile koti langu nyuma ya kiti, na fungua hapo kwenye droo yangu, utakuta kibunda cha pesa, pamoja na funguo ya gari. Tuwahi kwenda hospitali wasije wakakataa sisi kuingia”
“Sawa baba”
Magreth akaanza kutembea kwa hatua za haraka kuelekea ilipo meza hiyo. Makalio yake makubwa yanayo tetemeka mithili ya simu yenye vibration yakamfanya nabii Sanga kumeza fumba zito la mate, huku shetani wa ngono akiwa tayari amesha tawala kichwa chake. Nabii Sanga sasa akaanza kupata wakati mzuri wa kumchunguza Magreth. Moyo wake ukazidi kushangazwa na uzuri wa binti huyu ambaye siku zote amekuwa akimchukulia ni binti wa kawaida.
‘Umasikini wake ume ficha huu uzuri wake masikini weee’
Nabii Sanga alizugumza kimoyo moyo huku akimtazama Magreth jinsi anavyo rudi eneo alilo simama yaye. Magreth kwenye maisha yake yote hakuwahi kushuhudia pesa nyingi kama hizo. Akamkabidhi mchungaji vitu vyake.
“Ahaa binti yangu”
“Ndio baba”
“Sasa kama maandazi yako waliyamwaga. Utapata wapi mtaji mwengine wa kuendesha maisha yako?”
Swli hili likamfanya Magreth kukaa kimya na kushindwa kulijibu.
“Ila usijali, hilo nalo nitalitazama kwa jicho jengine na Mungu aweze kutusaidia ili tulipatie uvumbuzi”
“Asante baba mchungaji”
Wakatoka ofisini hapa. Nabii Sanga akafunga ofisi yake na kumuachia mlinzi wa kanisa hilo maagizo ya kuhakikisha kwamba awe makini katika ulinzi wa siku yake hiyo.
“Usijali nabii nitakuwa makini”
“Usije ukasinzia sinzia, kwa maana kuna siku huwa nina pitaga hapa usiku na kukuta ukiwa ume lala”
“Sinto sinzia mzee”
“Haya nifungulie geti”
Nabii Sanga alizungumza huku akifungua mlango wa gari lake hilo aina ya Toyota VX V8.
“Ka tu siti ya mbele”
Nabii Sanga alizungumza huku akimzuia Magreth kufungua mlango wa nyuma la gari lake. Wakaingia ndani ya gari na kuianza safari ya kuelekea hospitalini.
“Mage”
“Naam baba mchungaji”
“Nikikufungulia mgahawa, utaweza kuuandesha”
“Mgawaha!!?”
“Ndio mbona ume tahamaki?”
“Haki ya Mungu baba mchungaji nitakuwa nina fanya kazi kama mbwa. Sinto kuangusha katika hilo haki ya Mungu niamini katika hilo”
“Hahaaa usijali, ngoja kwanza”
Nabii Sanga akatoa simu yake mfukoni, akatafuta jina la moja wa dalali ambaye mara nyingi humtafutia nyumba kwa jiji hili la Dar es Salaam.
“Tomas”
“Shikamoo baba mchungaji”
“Marahaba. Hivi kwa maeneo ya Kinondoni tunaweza kupata ofisi ambayo ninaweza kufungua mgahawa?”
“Ahaa ndio mzee zipo sehemu nyingi sana pale, japo ada ya pango kidogo inakuwa juu”
“Kuhusiana na kodi hilo usiwe na shaka, wewe tafuta sehemu ambayo ina mzunguko mzuri wa biashara na niambie ni kiasi gani”
“Sawa baba mchungaji nitafanya hivyo”
“Hili swala usimuambie mama yako”
“Sawa mchungaji”
Nabii Sanga akakata simu huku akijawa na tabasamu pana usoni mwake. Magreth hakuamini kwamba ipo siku mambo yanaweza kubadilika kwa haraka namna hii hii. Maombi aliyo sali masaa kadhaa yaliyo pita hakika yana mfanya ajione ni mwenye bahati sana.
“Tomas akipata eneo hilo nitakujulisha.”
“Nashukuru baba mchungaji hakika Mungu amekuletea kwenye maisha yetu kwa makusudi sana”
“Usijali ehee kwenye hiyo nyumba una lipa kiasi gani kwa mwenzi?”
“Elfu kumi na tano?”
“Kumi na tano!!!?”
“Ndio na yule mama ana nidai kodi ya miezi miwili, kidogo biashara yangu imekuwa ngumu kutokana na hizi mvua mvua. Mbaya zaidi wale vijana wamenipora na pesa zangu hivyo basi sina chochote kilicho salia kwenye mifuko yangu.
“Ngoja tukipata hiyo sehemu ya mgahawa basi nitakupangishia nyumba maeneo hayo hayo ya kinondoni ili usiwe una pata shida ya kuelekea ofisini kwako”
“Ohoo asante Mungu, asante sana baba mchungaji”
“Usiwe na shaka katika hilo mwanangu”
Wakafika hospitalini na kutokana na umaarufu wa nabii Sanga, katika jiji la Dar es Saalam na Tanzania, walinzi na madaktari hawakusita kumruhusu kumuona mgonjwa.
“Hajazinduka hadi sasa?”
Nabii Sanga alizungumza huku wakiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi, alipo lazwa Evans.
“Hapana bado hajazinduka, tunatarajia kwenye majira ya saa nane usiku au alfajiri basi ana weza kuzinduka”
“Acha nimfanyie maombi, nina imani kwamba Mungu anaweza kufanya jambo katika hili. Dokta na wewe si dini yetu au wewe ni upande wa pili?”
“Mimi pia ni mkristo”
“Basi tuombe”
Wote watatu wakafumba macho na mchungaji Sanga akaanza kusali kwa sauti ya chini kidogo, kwani katika chumba hichi mtu haruhusiwi kupiga kelele.
“Amen”
Nabii Sanga mara baada ya kuzungumza neno hilo linalo ashiria kwamba sala imeisha, wakafumbua macho yao.
“Dokta nitalipa garama zote za huyu kijana anazo daiwa. Endapo kutatjitokeza haja ya kupelekewa hospitali kubwa basi mnifahamishe kwanza mimi”
“Sawa mchungaji, tutafanya hivyo”
“Hii ni business card yangu. Utawasiliana nami wakati wowote”
“Sawa sawa mchungaji”
“Mage nitakupeleka nyumbani na asubuhi utakuja hapa kumtembelea ili ufahamu maendeleo yake.”
“Sawa baba mchungaji”
Wakatoka kwenye chumba hichi cha wagonjwa. Nabii Sanga akalipa garama zote za matibabu kisha wakaanza safari ya kurudi nyumbani.
“Mage hivi una mchumba kwa maana sijawahi kusikia fununu pale kanisani kama kuna mchumba wako?”
Magreth akatabasamu huku akimtazama nabii Sanga kwa uso ulio jaa aibu aibu kidogo.
“Hapana baba mchungaji. Nina endelea kuulinda usichana wangu hadi pale Mungu atakapo nipatia mume wa kwangu peke yangu”
“Unataka kusema wewe bado hujawahi kutana kimwili na mwanaume?”
“Ndio baba mchungaji, bado mimi ni bikra”
Kauli hiyo ikaulipua moyo wa nabii Sanga, kwa umri wake wa miaka arobaini na sita hadi sasa, hajafanikiwa kukutana na mwanamke bikra na siku zote alikuwa akitamani sana kupata binti ambaye ni bikra kwani hata mke wake aliye muoa hakumkuta akiwa bikra.
ITAENDELEA
Haya sasa mambo ndio yanazidi kuwa matamu. Magreth amejihakikishia kupata utatuzi wa matatizo yake. Huku nabii Sanga naye akiamini kwamba maombi yake ya kumpata msichana bikra sasa Mungu amemfungulia je nini kitatokea? Endelea kufaatilia kisa hiki cha kusisimua, usikose sehemu ya 03